728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 24, 2017

    Watatu Serengeti Boys kwenda Ulaya kwa majaribio


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WACHEZAJI watatu wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania,Serengeti Boys waliokuwa nchini Gabon kwenye michuano ya AFCON wanatarajiwa kuondoka nchini mwezi ujao kwenda Ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani humo.

    Hilo limesemwa na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Alfred Lucas ambaye aliambatana timu hiyo huko nchini Gabon. 

    Lucas amesema vilabu vikubwa vya Hispania,Ubelgiji na Ufaransa vimeonyesha nia ya kutaka kuwasajili wachezaji wa Serengeti Boys baada ya kukoshwa na viwango walivyovionyesha kwenye michuano ya AFCON inayoendelea kutimua vumbi lake huko nchini Gabon.

    Lucas amewataja wachezaji hao kuwa ni Enrick Nkosi,Ally Msengi na Ally Ng'anzi.Hata hivyo Lucas hakutaja majina ya vilabu watakavyoenda kufanya majaribio vijana hao.



    Lucas ameongeza kuwa mpango huo umesukwa na Mtanzania,Abdallah Kondo ambaye ni wakala wa mshambuliaji mahiri wa Serengeti Boys,Yohana Mkomola ambaye nae anatarajiwa kwenda nchini Tunisia mwezi ujao kufanya majaribio ya kuchezwa soka la kulipwa kwenye klabu ya Etoile du Sahel.

    Wakati huohuo Serengeti Boys inatarajiwa kuwasili nchini leo mchana mishale ya saa 8:50 ikitokea nchini Gabon ambapo Jumamosi iliyopita kutolewa mashindanoni baada ya kufungwa bao 1-0 na Niger.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Watatu Serengeti Boys kwenda Ulaya kwa majaribio Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top