Dar es salaam,Tanzania.
Yanga Sc imemnasa mshambuliaji matata wa KMKM ya Zanzibar Matheo Antony Simon.Matheo ambaye alikuwa akipigiwa hesabu pia na klabu ya Simba SC amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuwachezea mabingwa wa Tanzania [Yanga] jana jumapili usiku.
Matheo alianza kunyatiwa na Simba SC baada ya kung'ara kwenye michuano ya Kagame kabla ya mapema wiki iliyopita kuifunga Simba SC magoli mawili katika mchezo wa kirafiki ambao KMKM ililala kwa bao 3-2.
0 comments:
Post a Comment