Manchester,England.
Hatimaye Manchester City imemsajili mlinzi Nicolas Otamendi kutoka Valencia baada ya zoezi la upimaji afya kufanikiwa.
Otamendi,27 amemwaga wino kuichezea Manchester City kwa kipindi cha miaka mitano baada ya Valencia kukubali ada ya £32m na atakuwa akivaa jezi namba 30.
Otamendi anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Manchester City msimu huu baada ya Raheem Sterling, Fabian Delph, Enes Unal na Patrick Roberts.
0 comments:
Post a Comment