728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 27, 2015

    HATIMAYE MAN UNITED YAREJEA LIGI YA MABINGWA ULAYA,ROONEY AMALIZA UKAME WA MECHI 10 BILA GOLI,MATOKEO NA TIMU ZILIZOFUZU VYOTE VIKO HAPA

    Manchester United imerejea tena katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya jana usiku kuibuka na ushindi mkubwa wa magoli 4-0 dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji.

    Manchester United ilijipatia magoli yake kupitia wa Wayne Rooney aliyefunga hat trik dakika za 20,49 na 57 huku goli la nne likifungwa na Ander Herrera dakika ya 63 kabla ya Chicharito kukosa penati dakika ya 81 ambayo ingeifanya Manchester United iondoke uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa goli 5-0.

    [Magoli hayo ya jana yanamfanya Rooney amalize ukame wa kutofunga goli katika michezo kumi iliyopita.Mara ya mwisho Rooney kuifungua Manchester United goli katika michezo rasmi ya kimashindano ilikuwa mwezi April mwaka huu]

    Kufuatia ushindi huo Manchester United inafuzu kwa jumla ya magoli 7-1 baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa magoli 3-1.Vilabu vingine vilivyofuzu usiku wa jana ni Bayer Leverkusen, CSKA Moskva, BATE Borisov na Astana huku Brugge,Lazio na vilabu vingine vilivyotolewa katika hatua hii vikiingia moja kwa moja katika ligi ndogo ya Ulaya maarufu kama (Europa Ligi).Makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa na Europa ligi itapangwa leo huko Monte Caro,Monaco ambapo pia mchezaji bora wa Ulaya kwa msimu uliopita atatangazwa.

    Matokeo mengine ya Agosti 26 ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo...

    Leverkusen 3-0 Lazio (agg: 3-1)
    APOEL 1-1 Astana (agg: 1-2)
    CSKA Moskva 3-1 Sporting CP (agg: 4-3)
    Partizan 2-1 BATE Borisov (agg: 2-2,BATE wamefuzu kwa faida ya goli za ugenini)

    Matokeo jumanne Agosti 25 ni kama ifuatavyo 

    Monaco 2-1 Valencia (agg: 4-5)
    Shakhtar Donetsk 2-2 Rapid Wien (agg: 3-2)
    Malmö 2-0 Celtic (agg: 4-3)
    Maccabi Tel-Aviv 1-1 Basel (agg: 3-3, Maccabi imefuzu kwa faida ya goli la ugenini)
    Dinamo Zagreb 4-1 Skënderbeu (agg: 6-2)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATIMAYE MAN UNITED YAREJEA LIGI YA MABINGWA ULAYA,ROONEY AMALIZA UKAME WA MECHI 10 BILA GOLI,MATOKEO NA TIMU ZILIZOFUZU VYOTE VIKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top