Manchester, England.
Wakati Pedro akiripotiwa kutua jijini London kufanyiwa vipimo vya afya kesho alhamisi katika klabu ya Chelsea,upande wa pili kunako klabu ya Manchester United habari zinadai kuwa klabu hiyo imeamua kujipoza na machungu ya kumkosa mkali huyo wa FC Barcelona kwa kuanza kumfukuzia nyota wa klabu ya Southampton Sadio Mane.
Mane,23 raia wa Senegal ameibukia kwenye orodha ndefu ya kocha Luis Van Gaal na tayari ameandaliwa kitita cha £15m baada ya Pedro Rodriquez aliyekuwa akiwindwa kwa kipindi kirefu kubadili mawazo dakika za mwisho na kuamua kutua Chelsea.
Mane nyota wa zamani wa klabu ya Red Bull Salzburg anatazamwa kama mbadala wa haraka wa Pedro baada ya msimu uliopita kuifungia Southampton jumla ya magoli kumi huku akiweka rekodi ya kufunga magoli matatu "Hat-Trik" ndani ya kipindi cha dakika 2 na sekunde 56.
0 comments:
Post a Comment