Roma,Italia
Wakati Chelsea ikipiga hesabu za kumnasa mlinzi wa Everton John Stones pia ilikuwa katika mawindo ya kuinasa saini ya mlinzi wa kati wa Stuttgart Mjerumani Antonio Rudiger.
Hizi ni saa za hatari na mbaya katika duru za usajili.Baada ya Jana jumatano Chelsea kuifanyia umafia Man United na hatimaye kumtia mkononi winga Pedro Rodriguez nayo imeporwa mlinzi Rudiger ambaye amejiunga na AS Roma ya Italia kwa mkopo wa msimu mmoja wenye thamani ya €4m kabla ya kuongeza nyingine €9m ili kummiliki moja kwa moja mlinzi huyo anayekipiga timu ya taifa ya Ujerumani.
Rudiger ameichezea Ujerumani jumla ya michezo 6 tangu alipoitwa kikosini kwa mara ya kwanza mwaka 2014 huku akifanikiwa kuivaa jezi ya Stuttgart mara 66.
Roma imemsajili Rudiger ili kuziba mapengo ya walinzi iliowauza Alessio Romagnoli kwenda AC Milan na Mapou Yanga-Mbiwa kwenda Lyon.
0 comments:
Post a Comment