Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua mwamuzi wa kati Martin Saanya kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii jumamosi, badala ya mwamuzi Israle Nkongo aliyekua amepangwa awali.
Mwamuzi Israel Nkongo anasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja, ambayo itampelekea kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha siku kumi, hali iliyopeleka TFF kumbadilisha mwamuzi huyo kuelekea kwenye mchezo huo wa jumamosi.
0 comments:
Post a Comment