728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 24, 2015

    WENGER:LIVERPOOL ILIKATAA KUTUUZIA SUAREZ SASA NIIHURUMIE ILI IWEJE?



    London,England.

    Wakati akitarajiwa kuiongoza klabu ya yake ya Arsenal kuivaa klabu ya Liverpool katika mchezo wa ligi kuu usiku wa leo kocha Arsene Wenge bado hajasahau maumivu ya kumkosa Luis Suarez baada ya Liverpool kukataa kata kata kumuuzia.

    Wenger alitaka kumsajili Suarez mwaka 2013 baada ya kutuma ofa ya £40,000,001 ambayo ndiyo ilikuwa ada halali ya kumnasa mshambuliaji huyo kwa mujibu wa kipengele kilichokuwa katika mkataba wake lakini Liverpool iliamua kumng'ang'ania nyota huyo na kisha msimu uliofuata ikamuuza FC Barcelona.

    Akiongelea usajili wa Raheem Sterling,Wenger amesema hana sababu ya kuihurumia Liverpool kwa kumpoteza nyota muhimu kama Sterling kwa kuwa klabu hiyo ya Anfield ilimfanyia mtimanyongo kwa kukataa kumuuzia Luis Suarez wakati alifikia dau lililokuwa linatakiwa.

    Wenger amesema "Liverpool wapo katika nafasi ambayo wanaweza kufanya maamuzi yao wenyewe.Walikataa kutuuzia Suarez,hivyo siwezi kuwahurumia kwa kuondokewa na Sterling".

    "Binafsi namkubali Raheem Sterling.Sidhani kama alikuwa akileta usumbufu.Ni katika kipindi cha usajili pekee ambapo mambo kama haya hutokea.

    "Wakati wa zoezi la usajili wake,Sterling alikuwa kimya hakuwahi kutoa kauli yoyote ya mbaya.Sidhani kama alikuwa mtu wa kelele nyingi.Ni mchezaji mzuri.Liverpool wamemsajili Firmino.Tutaona atakachokifanya.Ni mchezaji wa aina ile ile.

    "Lakini hebu tukumbuke miaka miwili iliyopita,Suarez, Sturridge na Sterling walifunga zaidi ya magoli mia moja.Kufunga magoli zaidi ya mia moja hapa [England] unahitaji vipaji maalum na Sterling alikuwa sehemu ya vipaji hivyo.Alimaliza Wenger
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WENGER:LIVERPOOL ILIKATAA KUTUUZIA SUAREZ SASA NIIHURUMIE ILI IWEJE? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top