Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amesema mazungumzo ya sekunde 60 pekee yalitosha kumshawishi winga Pedro Rodriguez aachane na FC Barcelona na kutua Stamford Blidge.
Akizungumzia jinsi alivyomnasa nyota huyo aliyekuwa akiwindwa na Manchester United kwa kipindi cha karibia mwezi mzima,Mourinho amesema "Ilinichukua dakika moja tu kumaliza kazi.
Kwa mujibu wa Mourinho mazungumzo yalikuwa hivi
"'Ni kweli kuwa unataka kuondoka FC Barcelona?' 'Ndiyo,Ni kweli.Napapenda.Ni nyumbani kwangu lakini inanibidi kuondoka' 'Je,Umeshasaini kujiunga na klabu yoyote ile?' 'Nimekaribia,lakini bado.Unataka kuja hapa?' 'Ndiyo,Nataka'
Nikakataa simu nikawaambia wenzangu kazi imeisha.
0 comments:
Post a Comment