ADAH WAIGAMA
Habari mpendwa msomaji wa makala zangu za kilimo,karibu katika mwendelezo wa makala yetu ya kilimo iliyopita iliyokuwa inaelezea mbolea na aina zake,leo tutaona namna ya kuandaa shamba na matumizi ya mbolea ya asili iliyotengenezwa kwa magugu ya majini na inaitwa Bio Plus.
Mavuno mengi pia yanachangiwa na maandalizi bora ya shamba kwanza kabisa andaa shamba lako kama lina magugu fyeka hayo magugu kisha yarundike pamoja ilikutengeneza mbolea,pili lima shamba lako kwa kutumia jembe la mkono, jembe la kukokotwa na ng'ombe(plau) au trekta kulingana na ukubwa wa shamba lako na uwezo wako wa kifedha ulionao.
Pili chagua aina bora ya mbegu kulingana na msimu na zao ulilopanga kupanda katika shamba lako, uchaguzi bora wa mbegu ni hatua ya pili katika kuelekea kuwa na mavuno mazuri katika mazao yako.
Tatu kama unatumia mbolea yoyote ya asili usipulize dawa ya kuua magugu katika shamba lako kwani dawa ya kuua magugu huua pia bakteria ambao hutumika katika kurutubisha ardhi.
MBOLEA YA BIO PLUS NI MIONGONI MWA MBOLEA ZA ASILI AMBAZO ZINATUMIKA KATIKA KILIMO NA ZIMEKUA NA MATOKEO MAZURI KATIKA KILIMO.
BIO PLUS ORGANIC SEA WEED FERTILIZER
Hii ni mbolea imetokanna na mimea au maotea ya majini. Hii ni mbolea ambayo ni ya asili kabisa kwani imetengenezwa kwa kuvundika mimea hii ya baharini na haina madhara kwa binadamu na mnyama yeyote na mazingira pia.
Hii mbolea inafaa kutumia kwa kuchanganya na viua wadudu vyovyote ambavyo ni aside au basic kwani utendaji kazi wake haudhuriki kabisa na kuchanganya mbolea hii na viua wadudu.
VIAMBATA VYA MBOLEA
1.Mbolea hii ina vichocheo vya mimea ambavyo ni asili kabisa kama AUXINS,CYTOKINS na GIBBERELLINS ambavo hivi ni VICHOCHEO VYA ASILI (NATURAL PLANT HORMONES) ambavo vina uwezo mkubwa wa kufanya mazao yako yaweze kumea vizuri na hatimaye mavuno mazuri
2.Mbolea hii ina madini zaidi ya sabini ambayo yana uwezo mkubwa wa kustawisha na kuimarisha mazao yako kwa kiwango cha juu kabisa.
KAZI ZA MBOLEA HII
1.Inaongeza uwezo wa mmea wako kuweza kufyonza madini na lishe mbali mbali kutoka kwenye udongo na pia kuotesha mizizi haraka
2.Inaongeza uwezo wa mimea yako kujitengenezea chakula chake wenyewe
3.Ina uwezo wa kuhifadhi unyevu nyevu katika udongo kwa muda mrefu
4.Inafanya mmea wako uweze kuhimili ukame,ubaridi na magonjwa mbali mbali
5.Inafanya mmea wako uweze kuota mapema kuongeza wingi wa mizizi na mimea kuwa na afya
6.Inaongeza kiwango cha mavuno ya mazao yako
7.Inaongeza muda wa matunda au mazao yako kukaa muda mrefu baada ya mavuno kama ukitumia hii mbolea siku kumi kabla ya kuvuna mazao yako.
MIMEA AMBAYO INASTAHILI MBOLEA HII
Mbolea hii inaweza kutumika katika mimea au mazao mbali mbali kwa mfano MATUNDA YOYOTE, MBOGA ZA MAJANI, MAZAO YA NAFAKA, DAWA ZA MITISHAMBA, MAUA,NYASI, PAMBA, NYANYA, HOHO, BILINGANYA, VITUNGUU NK
JINSI YA KUITUMIA MBOLEA
1.PAMBA
MATUMIZI
1.A. Unaweza kutumia kuloweka mbegu zako kabla ya kupanda
B. Chukua 40 mls za bioplus weka kwenye 20litres za maji. Inashauliwa kuwa utumie kiwango cha mbolea chenye kiwango cha 60 mls -90 ms kwa hekari moja. Loweka mbegu zako kwa masaa 5-10 ndipo uzitoe tayari kwa kupandwa.
2. wakati wa kutoa maua unashaliwa kutumia kiwango cha 180mls kwa hekari moja. Changanya 13-20mls za mbolea kwenye lita 20 za maji. Kasha nyunyuzia hiyo mbolea kwenye mazao yako.
2.MPUNGA
1.KULOWEKA MBEGU
Chukua 60-90 mls za mbolea ya bio plus kisha changanya kwenye lita ishirini ya maji. Hiki kiwango unaweza kubadili kulingana na lita za maji unazotumia hivyo unaweza tafuta ni kiasi gani cha mbolea unachohitaji kuchanganaya kwenye maji husika.Weka mbegu zako kwenye maji masaa manane mpaka kumi ndipo uzitoe tayari kwa kupandwa.
2.BAADA YA KUANZA KUTOA MAUA
Chukua 13-20 mls weka kwenye maji ya lita ishirini na kisha nyunyuzia mazao yako. Hakikisha kuwa hekari moja hauzidishi kiasi cha mbolea chenye wingi wa 240 mls kwa hekari moja.
3.MAHINDI
1.KULOWEKA MBEGU
Tumia 40mls za mbolea ya bioplus kuchanganya kwenye 20litre za maji. Kubuka hii ni kiwango kikubwa hivyo unaweza kutafuta kiwango cha mbolea kwa matumizi yako kwa mfano lita tano utahitaji kiwango cha mbolea kiasi gani? Weka mbegu zako ndani ya mbolea kwa muda wa masaa 8-10
2.MAHINDI YAKISHATOA MAJANI,MAUA
CHUKUA 20 mls za mbolea weka kwenye maji 20litres kisha nyunyuzia mahindi yako. Usizidishe 720mls za mbolea kwa hekari moja.
4.MBOGA ZA MAJANI
Chukua 40mls za mbolea kisha weka kwenye lita 20 za maji na nyunyuzia mboga zako. Unashauliwa usizidishe 720 mls za mbolea kwa hekari moja. Unaweza nyunyuzia mara tatu kwa kipindi chote.
5.TANGO,TIKITI NA NYANYA
Chukua 20mls za mbolea changanya na 20 litres za maji na kisha nyunyuzia. Unashauliwa usizidishe kiasi cha 720mls kwa kila hekari kila unaponyunyuzia hii mbolea. Unaweza kunyunyuzia hadi mara tatu hadi kufikia mazao yako kuvuna.
PIA UNAWEZA KUITUMIA KWA MAZAO KAMA APPLE,NDIZI,MAEMBE, ULIMAJI WA SOYA NK.
KUMBUKA.
1.Mbolea iliyochanganywa na maji itumike ndani ya masaa 24 tu.
2.muda wa kupulizia ni asubuhi mpaka saa tatu na kuanzia saa kumi jioni
3.kama mvua itanyesha wakati umemaliza kunyunyuzia itabidi urudie upya kupulizia mbolea katika mazao yako, mmea unatakiwa ukae masaa sita bila mvua.
KWA MAELEZO ZAIDI NA NAMNA YA KUIPATA MBOLEA USISITE KUWASILIANA.
+255 787 218 159
+255 764 218 159
0 comments:
Post a Comment