Baada ya goli lake kukataliwa kwa madai kwamba alikuwa ameotea kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey amekitaka chama cha soka England kutumia picha za televisheni kuamua matokea michezoni.
Ramsey ameyasema hayo baada ya goli alilolifunga katika mchezo wa ligi kuu jana jumatatu dhidi ya Liverpool kukataliwa.
Malalamiko hayo ya Ramsey yanakuja baada ya picha za televisheni kuonyesha kuwa kiungo huyo hakuwa ameotea kama mwamuzi alivyodai.Picha hizo zinamuonyesha Rasmsey akiwa sambamba na mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel wakati akipokea pasi ya Santi Cazorla na kumfunga mlinda mlango Simon Mignolet.

Amesema "Kutazama video kwa sekunde 20 nadhani kungebadili matokeo ya mchezo,"
"Tunaweza kujifunza kutoka kwenye mchezo wa rugby.Wanfanya vizuri sana."Unaona kwenye televisheni,wanatazama kwa sekunde 20 kujiridhisha kisha wanatoa uamuzi sahihi.Soka linaweza kujifunza kitu kutoka huko." Alimaliza Ramsey.
Malalamiko hayo ya Ramsey yanakuja baada ya picha za televisheni kuonyesha kuwa kiungo huyo hakuwa ameotea kama mwamuzi alivyodai.Picha hizo zinamuonyesha Rasmsey akiwa sambamba na mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel wakati akipokea pasi ya Santi Cazorla na kumfunga mlinda mlango Simon Mignolet.
0 comments:
Post a Comment