728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 20, 2015

    HADITHI YA MAN CITY NA OTAMENDI INAELEKEA KUTAMU,SOUTHAMPTON YATOA TAMKO KUHUSU MANE

    Kutoka Daily Mirror habari zinasema mlinzi wa Valencia Muargentina Nikolas Otamendi leo alhamisi atatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Manchester City baada ya jana jumatano kufanyiwa vipimo vya afya katika makao makuu ya klabu hiyo.

    Otamendi,27 ambaye ameiingizia Valencia £32 katika dili hilo atasaini mkataba wa miaka mitano na kuwa nyota wa tano kujiunga na klabu hiyo inayokipiga katika dimba la Etihad baada ya Raheem Sterling, Fabian Delph, Enes Unal na Patrick Roberts.

    Baada ya kumalizana na Otamendi,Manchester City itafunga usajili wa kumleta kiungo wa Wolfsburg Mbelgiji Kevin De Bruyne.

    Upande wa pili Manchester United imeambiwa ikae mbali na winga Southampton Msenegal Sadio Mane kwani klabu hiyo ya St.Mary's haina mpango wa kumuuza nyota wake huyo mwenye miaka 23.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HADITHI YA MAN CITY NA OTAMENDI INAELEKEA KUTAMU,SOUTHAMPTON YATOA TAMKO KUHUSU MANE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top