Mario Balotelli amerejea nyumbani AC Milan katika klabu aipendayo kuliko kitu chochote kile katika maisha yake ya soka.Lakini wakati akiamua kurudi San Siro mabosi wa klabu hiyo kongwe na kubwa Italia na Ulaya wameamua kumbana Balotelli kwa kuhakikisha kuwa nyota huyo aliyetua klabuni hapo kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Liverpool haleti matata baada ya ripoti kutoka Italia zikidai kuwa AC Milan imemuwekea nyota huo utitiri wa masharti ya kufuata vinginevyo atarudishwa Liverpool mara moja.
Sehemu ya masharti hayo ni hii
- Kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram itakuwa ikifuatiliwa kwa karibu zaidi ili asije akachafua jina na hadhi ya klabu.
- Kuachana na unyoaji nywele wa ajabu ajabu’
- Mavazi yaendane na hadhi ya AC Milan siyo kuvaa hovyo hovyo
- Kupunguza uvutaji wa sigara
- Kuwahi mapema mazoezini na popote pale atakapohitajika na klabu huku akipigwa marufuku kukanyaga katika kumbi za starehe
0 comments:
Post a Comment