Madrid,Hispania.
Real Madrid imepata ushindi wake wa kwanza wa La Liga baada ya kuifumua Real Betis kwa jumla ya mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu.
Real Madrid ambayo katika mchezo wa kwanza wa La Liga ilibanwa mbavu na kulazimishwa sare tasa na Sporting Gijon ilionekana mapema kuizidi maarifa Betis baada ya kupata bao dakika ya (2) tu ya mchezo baada ya Gareth Bale kufunga kwa kichwa,dakika ya 39 James Rodriguez alifunga la pili kabla ya Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 47 kisha James Rodriguez dakika ya 50 na mwisha Gareth Bale dakika ya 89.
Katika mchezo mwingine FC Barcelona ilisubiri mpaka dakika ya 73 iweze kuishinda Malaga baada ya mlinzi Thomas Vermaelen kufunga goli kwa shuti kali la karibu.
0 comments:
Post a Comment