Unaikumbuka fainali ya kombe la dunia la mwaka 1986?Unalikumbuka goli la mkono wa Mungu aliliolifunga Maradona katika mchezo wa robo fainali dhidi ya England katika dimba la Azteca?Unamkumbuka mwamuzi aliyechezesha mpambano ule?Kama umesahau anaitwa Ali Bennaceur raia wa Tunisia.
Sasa mapema wiki hii wawili hao walikutana jijini Tunis ambapo Maradona alikwenda kutengeneza tangazo la biashara.Baada ya Maradona kumuona Ali alimfuata akamkumbatia na kumpiga mabusu yasiyo na idadi na kisha kumkabidhi jezi ya Argentina ikiwa na saini yake pamoja na maandishi yaliyosomeka "Ali rafiki yangu wa ndani"
Ali,hakuzubaa nae akajibu mapigo kwa kumpa Maradona picha inayomuonyesha yeye (Ali),Maradona na mlinda mlango wa England siku ile Shilton,waliyopiga pamoja katika dimba Azteca Stadium,Mexico kabla ya kuanza kwa mchezo ule.
0 comments:
Post a Comment