Baada ya kubwagwa katika mchezo wa Super Cup hatimaye leo FC Barcelona imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Athletic Bilbao baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Bao pekee la mchezo huo uliojaa ubabe,majeruhi na makosa ya mwamuzi limefungwa dakika 54 na mshambuliaji Luis Suarez akimalizia kazi nzuri ya mlinzi Jordi Arba huku mchezaji Lionel Messi akiinyima FC Barcelona bao la mapema baada ya mkwaju wake wa penati kuokolewa wa mlinda mlango wa Bilbao Iraizoz.
Mpaka sasa Messi ameshakosa penati 14 kati ya 63 alizopiga akiwa na FC Barcelona huku goli la leo likimuwesha katika nafasi nzuri mshambuliaji Luis Suarez ya kuweza kutwaa tuzo ya mfungaji bora [Pichichi] mwishoni mwa msimu ikiwa ataendelea kufunga.
VIKOSI
Barcelona: Bravo; Alves (Roberto), Mascherano, Vermaelen, Alba; Busquets (Bartra), Rakitic, Iniesta; Messi, Suárez, Rafinha (Sandro)
Athletic: Iraizoz; De Marcos, Elustondo, Laporte, Balenziaga (Bóveda); Mikel Rico (Gurpegi), Beñat, Eraso; Susaeta, Aduriz, Sabin Merino (Ibai Gómez)
Mwamuzi:Del Cerro Grande
0 comments:
Post a Comment