Kikosi cha Taifa Stars kitaendelea na mazoezi leo kwenye Viwanja vya Hoteli ya The Green Park nchini Uturuki.Chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa, Stars jana ilifanya mazoezi kama kawaida kwenye viwanja hivyo ambako imeweka kambi kuiwinda Nigeria katika mechi itakayochezwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.Stars ilifanya mazoezi mara moja baada ya mazoezi mfululizo tena yale makali.
Leo pia inatarajia kufanya mazoezi mara moja kwa kuwa kesho kikosi hicho kitashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki ya mazoezi dhidi ya timu ya taifa ya Libya.Mazoezi ya Stars yamekuwa
yakiendelea katika eneo hili ambalo kila nyakati za jioni kunakuwa na hali ya baridi kali pamoja na ukungu.Hata hivyo wachezaji wa Stars wamekuwa wakipata nafasi ya kupumzika vizuri kutokana na mazingira ya eneo husika.
Eneo hili ni kwa ajili ya timu zinazoweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali.Hakuna sehemu za starehe zaidi ya michezo mbalimbali,viwanja vya michezo na sehemu nzuri za kula tu.
0 comments:
Post a Comment