728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 23, 2015

    WAKENYA HOI BEIJING,WACHEMSHA VIBAYA MARATHON

    Wanariadha wakenya waliambulia patupu katika mashindano ya mbio za marthon za kufungua makala ya mwaka huu ya mashindano ya riadha ya dunia huko Beijing China.

    Tineja kutoka Eritrea , Ghirmay Ghebreslassie, ndiye aliyeizolea Eritrea dhahabu ya kwanza ya makala ya 15 ya mashindano haya aliposajili muda bora wa saa mbili na dakika kumi na mbili(2:12:27).

    Ghebreslassie alitoka nyuma na kumpiku mwanariadha kutoka, Lesotho Tsepo Ramonene, katika hatua ya kilomita 42 .

    Wakati huo Yemane Tsegay, wa ethiopia ndiye aliyekuwa ameshindwa na kasi na joto iliyokuwa imewazidi wanariadha wengi watajika.

    Tsegay hatimaye aliridhika kwa nishani ya fedha alipomaliza mbio hizo akiandikisha muda wa saa mbili 2:13:07.

    Mwanariadha kutoka Uganda Solomon Mutai (2:13:29)ndiye aliyetamatisha orodha ya tatu bora na kuwanyamazisha wakenya ambao walikuwa wamepigiwa upatu kusajili muda bora na kutawala mbio hizo za kwanza katika uwanja wa Birds Nest ulioko Beijing.Amini usiamini,mwanariadha wa kwanza raia wa Kenya alimaliza mbio hizo katika nafasi ya 22 naye alikuwa ni bingwa wa mbio za Paris Marathon Mark Mutai.

    Aliandikisha muda wa saa mbili na dakika 21. 2:21:19 .Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo Kenya ilikuwa imewasilisha kikosi kilichojumuisha mshikilizi wa rekodi ya dunia.

    Dennis Kimetto (2:02:57), Bingwa wa mbio za Marathon za Chicago na vilevile Berlin, Wilson Kipsang (2:03:23) na vilevile mshindi wa mbio za marathon za London na New York.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAKENYA HOI BEIJING,WACHEMSHA VIBAYA MARATHON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top