Manchester,England.
Manchester United imekubali dau la £12m usiku wa jana toka Bayer Leverkusen kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake Mmexico Javier Hernandez "Chicharito".
Kutoka Daily Mail habari zinapasha kuwa jumatatu/jumanne Chicharito,27 atasaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea miamba hiyo ya Ujerumani baada ya hivi karibuni kuambiwa na kocha Luis Van Gaal kuwa hayumo katika mipango yake.
Kuondoka huko kwa Chicharito kunaifanya Manchester United ibaki na washambuliaji wawili tu katika kikosi chake ya wakubwa.Washambuliaji hao ni Wayne Rooney na James Wilson.
0 comments:
Post a Comment