728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 30, 2015

    TUMEMCHUKUA!!DE BRUYNE ASAINI MIAKA SITA MAN CITY,REKODI MPYA YAWEKWA,AAHIDI MATAJI ZAIDI

    Manchester City imeendelea kuonyesha kuwa inayajua matumizi sahihi ya pesa baada ya leo kumnasa kiungo Mbelgiji Kevin De Bruyne kwa kitita cha rekodi cha paundi milioni 54 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani.De Bruyne anarejea tena England ukiwa ni msimu mmoja tu tangu aihame Chelsea na kutua Wolfsburg kwa ada ya paundi milioni 18 baada ya kutibuana na Kocha Jose Mourinho.

    MAN CITY YAWEKA REKODI
    kev

    Manchester City sasa imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya England kuwahi kutumia pesa nyingi zaidi katika kipindi cha usajili ikiipiku rekodi iliyowekwa msimu uliopita na majirani zao wa jiji la Manchester klabu ya Manchester United waliotumia paundi milioni kwa kuwasajili Angel di Maria, Ander Herrera na Luke Shaw,
                          kev
    Baada ya kumnasa De Bruyne Manchester City inafikisha paundi milioni 160 baada ya kuwasajili De Bruyne, Raheem Sterling, Nicolas Otamendi, Fabian Delph, Patrick Roberts na Enes Unal na kushika nafasi ya pili kidunia nyuma ya Real Madrid ambayo mwaka 2009 ilitumia paundi 195 kuwasajili Cristiano Ronaldo, Kaka na  Karim Benzema .
    kev
    Akiongea baada ya kujiunga na City De Bruyne amesema ametua tena England kwa kuwa ligi yake ni bora zaidi dunia na anataka kuendelea kushinda mataji baada ya msimu uliopita kuisaidia Wolfsburg kushinda mataji mawili.
    kevkev

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TUMEMCHUKUA!!DE BRUYNE ASAINI MIAKA SITA MAN CITY,REKODI MPYA YAWEKWA,AAHIDI MATAJI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top