Everton imemsajili mshambuliaji wa River Plate Montevideo ya Uruguayi Leandro Rodriguez.Rodriguez amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia miamba hiyo ya Goodison Park,Everton imegoma kutaja kiasi cha pesa ilichotumia kumnasa nyota huyo mwenye miaka 22.
Sunderland imemsajili kwa mkopo wa msimu mmoja kiungo MSweden Ola Toivonen toka klabu ya Rennes ya Ufaransa.Toivonen,29 ameifungia Rennes jumla ya magoli 14 katika michezo 46
Tottenham imemsajili mshambuliaji Mkorea Heung-Min Son toka Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa ada ya paundi milioni 17.Son amesaini mkataba wa miaka mitano na amekabidhiwa jezi namba 7 kinachosubiriwa kwa sasa ni kupatikana kwa kibari cha kufanyia kazi England.
Akiwa na Leverkusen Son,23 amefunga magoli 29 katika michezo 87 huku akifunga mengine matatu katika michuano ya ligi ya mabungwa Ulaya msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment