Dar es salaam,Tanzania.
Mashabiki wa Simba SC waliokuwa na hamu kumuona kwa mara nyingine straika Mrundi Kevin Ndeyisenga akivaa jezi ya klabu yao na kufunga tena bao kama lile alilofunga katika mchezo dhidi ya URA hawataipata tena fursa hiyo kwani nyota huyo wa Vital'O ameshindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Simba SC na tayari amerudi kwao.
Ndayisenga alitua Simba SC kuja kujaribu bahati yake lakini kwa bahati mbaya dau la dola 70,000 lililohitajika ili kumbakisha mitaa ya Msimbazi limekataliwa na Simba kwa madai kuwa ni kubwa mno.Simba ilikuwa tayari kutoa dola 30,000 pekee kama ada ya uhamisho na mambo mengine lakini baada ya kuambiwa itoe dola 70,000 ndipo iliporuka kimanga na kuamua kuachana na straika huyo.
Mchanganuo wa Dola 70,000 uko hivi,Vital'O ilitaka ilipwe dola 35,000,Wakala dola wake 15,000 na Ndayisenga mwenyewe achukue dola 20,000.
0 comments:
Post a Comment