728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 25, 2015

    ARSENAL,LIVERPOOL HAKUNA MBABE ZASHINDWA KUFUNGANA EMIRATES,MAKIPA WAZIBEBA TIMU MGONGONI



    London,England.

    Vilabu vya Arsenal na Liverpool vimetoka sare ya bila kufungana katika mchezo pekee wa ligi kuu England uliopigwa usiku wa jumatatu katika dimba la Emirates katika mchezo ambao makipa walifanya kazi nzuri na kuvinusuru vilabu vyao na kipigo.

    Arsenal ikicheza kwa mara ya kwanza bila ya Per Mertesacker na Laurent Konscienly katika idara ya ulinzi ilifanikiwa kupata bao dakika ya tisa ya mchezo lakini mwamuzi Michael Oliver alikataa bao hilo kwa madai kuwa mfungaji wa bao hilo Aaron Ramsey alikuwa ameotea.

    Shukrani za dhati ziwaendee makipa Peter Cech na Simon Mignolet kwa kusimama imara malangoni mwao na kuokoa michomo ya hatari.Cech aliinusuru Arsenal mara isifungwe baada kuokoa michomo ya Felipe Coutinho na Christian Benteke huku Mignolet akiinyia Arsenal ushindi kwa kuokoa mashuti ya Alexis Sanchez na Oliver Giroud.

    Kufuatia matokeo hayo Arsenal inafikisha alama nne huku Liverpool wao wakifikisha alama saba baada ya vilabu vyote kuwa vimeshuka dimbani mara tatu.James Milner alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo 

    Vikosi vilivyoshuka dimbani...

    Arsenal (4-2-3-1): Cech, Bellerin, Gabriel, Chambers, Monreal, Coquelin (Oxlade-Chamberlain 82), Cazorla, Ramsey, Ozil, Sanchez, Giroud (Walcott 73)

    Liverpool (4-1-4-1): Mignolet, Clyne, Skrtel, Lovren, Gomez, Lucas (Rossiter 75), Firmino (Ibe 62), Milner, Can, Coutinho (Moreno 88), Benteke.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL,LIVERPOOL HAKUNA MBABE ZASHINDWA KUFUNGANA EMIRATES,MAKIPA WAZIBEBA TIMU MGONGONI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top