Kigali,Rwanda.
Kitua cha luninga cha Azam TV kimeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini ligi kuu ya nchini Rwanda.
Mkataba huo wenye thamani ya dola milioni 2.35 ulisainiwa jana jumatatu huko Remera,Kigali katika makao makuu ya chama cha soka cha nchi hiyo kiitwacho FERWAFA.
Kufuatia kusainiwa kwa mkataba huo ligi kuu ya Rwanda itakuwa ikijulikana kama Azam Rwanda Premier League.
Kabla ya Rwanda,Azam TV tayari ilishaanza kuzidhamini ligi kuu za Tanzania, Uganda, Burundi na ligi daraja la pili ya Kenya.
0 comments:
Post a Comment