Leo ni Leo huko Monte Caro,Monaco ambapo licha ya kufanyika upangaji wa makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya (Champions Ligi) na Europa Ligi kitimutimu kingine kitakuwa ni kumpata mchezaji bora wa Ulaya kwa msimu wa 2014/2014.
Wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Lionel Messi (FC Barcelona),Luis Suarez (FC Barcelona) na Cristian Ronaldo (Real Madrid) ambao wameingia hatua hiyo baada ya kuwabwaga nyota kibao wakiwemo Gianluigi Buffon (Juventus),Neymar (Barcelona),Eden Hazard (Chelsea),Andrea Pirlo (Juventus),Arturo Vidal (Juventus/Bayern München),Carlos Tévez (Juventus,/Boca Juniors),Paul Pogba (Juventus).
Wachambuzi wengi wa masuala ya soka wanampa nafasi Lionel Messi kutwaa tuzo hiyo mbele ya Ronaldo na Suarez.Messi aliifungia FC Barcelona magoli 58 na kuipa mataji ya La Liga,Champions Ligi,Copa De Rey na Uefa Super Cup huku Ronaldo akiishia kufunga magoli 61 bila ya kutwaa taji lolote.
Wachezaji waliowahi kutwaa tuzo hiyo miaka ya karibuni ni Lionel Messi (2011) , Andrés Iniesta (2012) , Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014)
0 comments:
Post a Comment