Munich,Ujerumani.
Wakati Manchester City ikijiandaa kumtangaza Kevin De Bruyne kuwa mchezaji wake mpya baada ya kufaulu vipimo vya afya siku ya jana jumamosi taarifa toka Ujerumani zinadai kuwa kampuni ya kutengeza magari ya Volkswagen ambayo inaidhamini Wolfsburg ilitaka kukwamisha usajili huo.
Taarifa za kuamini zinadai kuwa kampuni ya Volkswagen iliitaka Wolfsburg imuuze De Bruyne kwenda Bayern Munich badala ya Manchester City lakini mpango huo haukufanikiwa baada ya Bayern Munich kushindwa kufikia dau lililokuwa likitakiwa na Wolfsburg ili imuachie nyota huyo wa Ubelgiji.
Habari zinazidi kupasha kuwa shinikizo hilo lilitoka kwa mwenyekiti wa kampuni ya Volkswagen bwana Martin Winterkorn ambaye ni mmoja kati ya wakuu wa bodi ya Bayern Munich hivyo alitaka kutumia ushawishi wake ili kukwamisha dili hilo.
0 comments:
Post a Comment