728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 28, 2015

    EVERTON JEURI WEWE:YAIPIGA CHINI CHELSEA,YAMPIGA CHINI JOHN STONES,MASHABIKI WAJA JUU,AHAMIA HOTELINI

    Liverpool,England.

    Chelsea inamtaka John Stones.John Stones nae anaitaka Chelsea.Chelsea na John Stones wanatakana.Hii ndiyo hali halisi.Everton haitaki fedha za Chelsea.Everton haitaki kumpoteza John Stones.Everton imeipiga chini ofa ya nne ya £37m toka Chelsea.

    Sasa ni rasmi kuwa klabu ya Everton haitamuuza mlinzi wake mahiri wa kati John Stones kwenda Chelsea ama klabu nyingine licha ya nyota huyo wa England (U-21) kuilima klabu hiyo barua ya kuomba kuondoka.

    John Stones,21 mapema siku ya jumanne ya wiki hii aliilima barua klabu hiyo ya jiji la Liverpool akiomba kuondoka ili aweze kujiunga na klabu ya Chelsea.Stone alifikia hatua hiyo baada ya kuona Everton ikiendelea kuzikataa ofa zote kutoka Chelsea.

    Uongozi wa juu wa Everton baada ya kuisoma barua hiyo lakini bado umeshikiria msimamo wake ule ule na kuendelea kusisitiza kuwa mlinzi huyo hauzwi kwa gharama yoyote ile.Aliyeanza kuupangua mpango huo ni meneja Roberto Martinez kabla ya mwenyekiti Bill Kenwright kuongeza kuwa Everton inajivunia kuwa na nyota kama John Stones hivyo suala la kumuuza litabaki kuwa ni ndoto za mchana.

    Wakati huohuo habari za chini chini zinadai tangu Stones aanze kulazimisha kujiunga na Chelsea amejikuta katika wakati mtu kufuatia baadhi ya mashabiki wa Everton kupanga kumfanyia kitu mbaya nyota huyo hali iliyofanya Stones aikimbie nyumba yake na kuanza kuishi hotelini.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EVERTON JEURI WEWE:YAIPIGA CHINI CHELSEA,YAMPIGA CHINI JOHN STONES,MASHABIKI WAJA JUU,AHAMIA HOTELINI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top