London,England.
Meneja Jose Mourinho amesema Chelsea ilikuwa sahihi kumuuza winga wake wa zamani Kevin de Bruyne kwenda Wolfsburg ya Ujerumani mwaka 2014.
Mourinho ameyasema hayo wakati ambapo kuna taarifa kuwa nyota huyo huenda akajiunga na Manchester City akitokea Wolfsburg kwa ada ya rekodi ya £50m.
Akinukuliwa na Sky Sports Mourinho amesema
"Ukiwa na mchezaji anayekuja kila siku kukugongea mlango huku akilia kuwa anataka kuondoka,unapaswa kufanya maamuzi"
"Kama De Bruyne angebaki hapa,hana furaha na hana motisha na kisha tungemuuza mwaka mmoja baadae,tungepata asilimia 50 pungufu ya bei tuliyomuuzia".
Mourinho ameongeza "Bruyne hakuwa tayari kushindana.Alikuwa ni kijana aliyejaa chuki,akifanya mazoezi hovyo hovyo.Hatukuwa na jinsi nyingine ya kumsaidia zaidi ya kumuuza"
0 comments:
Post a Comment