Kipa Juma Kaseja amesaini mkataba wa miezi sita wa kuichezea klabu ya Mbeya City yenye makao makuu yake mkoani Mbeya.Kaseja amesaini mkataba huo jana jumatano mbele ya meneja wake mpya, Athumani Tippo pamoja uongozi wa Mbeya City.
Taarifa za kuaminika zinadai mlinda mlango huyo mkongwe aliyewahi kuvichezea vigogo vya soka la Tanzania Simba na Yanga amesaini mkataba huo jijini Dar es Salaam.Kaseja anajiunga na Mbeya City baada ya kuwa ameitumikia Yanga kwa kipindi kifupi kabla ya kuingia mitini baada ya kutoridhishwa na mambo flani flani.
0 comments:
Post a Comment