Hekaheka za usajili barani Ulaya zimeendelea kupamba moto baada ya vilabu vya Hispania na Italia kuendelea kuimarisha vilabu vyao.
|
Lukas Digne amejiunga na AS Roma akitokea Monaco kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja akichukua nafasi ya Ashley Cole |
Asier Illarramendi amejiunga na Real Sociedad kwa ada ya Euro 17m akitokea Real Madrid
Fabio Coentrao ameihama Real Madrid na kujiunga na Monaco kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja kwenda kuziba nafasi ya Lyvin Kurzawa anayejiandaa kwenda PSG.
Fernando Llorente amejiunga na Sevilla akitokea Juventus baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.Llorente amesaini mkataba wa miaka minne.
0 comments:
Post a Comment