728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 23, 2015

    NI SHEEEDAH!!VICTOR WANYAMA AANZA KUIKERA SOUTHAMPTON

    Southampton,England.

    Kiungo Mkenya Victor Wanyama ameiambia klabu yake ya Southampton kuwa anataka kutimka St.Mary's kabla ya dirisha la usajili nchini England halijafungwa mapema mwezi ujao.

    Kauli hii ya Wanyama,24  imekuja siku moja tu baada ya siku ya ijumaa kocha wake katika klabu ya Southampton Ronald Koeman kusema kuwa nyota huyo hauzwi.

    Habari za kuaminika zinadai kuwa Wanyama amewambia  viongozi wa ngazi za juu wa klabu hiyo kuwa amekuwa hana furaha klabuni hapo kwa kipindi kirefu sasa na hayuko tayari kusaini mkataba mpya licha ya kubakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa.Inasemekana Wanyama anataka kutua Tottenham kuungana na kocha wake wa zamani Mauricio Pochettino.

    Wanyama alijiunga na Southampton mwaka 2013 kwa ushawishi wa kocha Mauricio Pochettino kwa ada ya rekodi ya £12.5m akitokea Celtic ya Scotland kabla ya hapo alikuwa akiichezea Beerschot AC ya Ubelgiji.

    Mpaka sasa Wanyama ameichezea Southampton michezo 57 na kufanikiwa kuifunga magoli matatu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NI SHEEEDAH!!VICTOR WANYAMA AANZA KUIKERA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top