England
West Bromwich Albion imefanikiwa kumsajili mlinzi John Evans toka Manchester United kwa mkataba wa miaka minne huku ada ya uhamisho ikifanywa siri.
Evans,27 amejiunga na West Brom usiku huu baada ya kufuzu vipimo vya afya alivyofanya siku ya ijumaa.Ujio huo wa Evans aliyefanikiwa kucheza jumla ya michezo 196 akiwa Manchester United kunatoa nafasi kwa mlinzi Joleon Lescott anayetarajiwa kuihama West Brom na kujiunga na Aston Villa kwa kitita cha £2m.
Atletico Madrid [Rojiblancos] imemsajili kiungo Matias Kranevitter "El Caddy" toka River Plate ya Argentina kwa ada ya uhamisho ya €8m.
Kranevitter,22 maarufu kwa jina la "El Caddy" amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia miaka hiyo ya Vicente Cardelon baada ya kupata pasi ya kusafiria.
Kranevitter ambaye kiuchezaji anafananishwa na kiungo wa FC Barcelona Javier Mascheranno ataanza kuitumikia Atletico Madrid mwezi Desemba 30 itakapokuwa ikivaana na Rayo Vallecano katika mchezo wa ligi ya La Liga.Hilo limefikiwa baada ya River Plate kuiomba Atletico Madrid imruhusu Kranevitter aisaidie timu katika michuano ijayo ya kombe la dunia la vilabu litakalotimua vumbi mwishoni mwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment