Uongozi wa klabu ya Simba
umeamua kuchana na Wasenegali wote na sasa inamrudisha Kelvin Ndayisenga.
Ndayisenga raia wa Burundi
alifanya majaribio Simba akafuzu lakini ikawa tatizo katika suala la
makubaliano ya kifedha.Pamoja na kutaka dau la zaidi ya Sh milioni 80,Ndayisenga alitaka alipwe Sh 200,000 kwa kila bao atakalofunga.
Simba ikaamua kuachana
naye na kumleta Papa Niang
kutoka Senegal ambaye alishindwa kuonyesha uwezo.
Aliposhindwa, ikamshusha Abdoulaye Nd’aw ambaye pia alionyesha hana lolote baada ya kuanguka mazoezini akionekana hayuko fiti.
Taarifa zinaendeleza Ndayisenga anarejea Dar es Salaam kujiunga na Simba baada ya Simba kukubaliana na wakala wake, Denis Kadito, Mtanzania anayeishi nchini Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment