728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 25, 2015

    BAADA YA KUTUA AC MILAN,MARIO BALOTELLI AAHIDI KUACHA MIGUU IONGEE

    MKOPO!!Mario Balotelli ametua tena AC Milan akitokea Liverpool kwa uhamisho wa mkopo baada ya kuihama mmoja msimu uliopita.Balotelli amekuwa na msimu mbaya zaidi Liverpool  mpaka kufikia kuondolewa kikosini na kulazimishwa atafute timu mpya ili akarudishe kiwango chake.

    Akiongea na waandika wa habari mara baada ya kukamilisha vipimo vya afya katika klabu ya Milan Balotelli amesema "Nataka kujifua na kuonyesha kile ninachoweza kufanya … nahitaji kujituma sana na kuacha miguu yangu iongee uwanjani badala ya mdomo."

    Balotelli hajacheza mchezo wowote wa kimashindano kwa miezi minne sasa baada ya kocha Brendan Rodgers kupoteza imani kufuatia kuonyesha kiwango cha chini sana kwani amefanikiwa kufunga magoli manne tu tangu alipojiunga na Liverpool mwaka 2014.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUTUA AC MILAN,MARIO BALOTELLI AAHIDI KUACHA MIGUU IONGEE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top