London,England.
Baada ya kuifungia bao klabu yake mpya ya Chelsea na kisha kutengeneza jingine winga Pedro Rodriguez amemwagiwa sifa kibao na kocha wake mpya Mreno Jose Mourinho.
Akiongea baada ya kuiongoza klabu yake kuibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya West Brom Albion kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameenda mbali zaidi na kumfananisha winga wake Pedro na gwiji wa zamani wa soka wa Argentina Diego Maradona.
Pedro aliyejiunga na Chelsea siku ya alhamisi akitokea FC Barcelona kwa ada ya £21m alianza katika kikosi cha kwanza kilichoshuka dimbani jana jumapili katika dimba la ugenini la Hawthorns kusaka ushindi wa kwanza wa ligi kuu alifunga bao lake la kwanza EPL dakika ya 20 na kisha kutengeneza jingine dakika ya 30.
Baada ya Pedro kuonyesha Kiwango hicho bora kilichompatia tuzo ya mchezaji bora wa mechi kocha Mourinho ameshindwa kuzuia furaha yake amesema ni wachezaji wachache sana wanaoweza kuja katika ligi mpya na ngumu kama ya England na kisha kufanya alichokifanya Pedro.
Mourinho amesema "Siyo kama Maradona moja kwa moja lakini alikaribia.Ni mchezaji mzuri.Kila siku kuna swali kuhusu wachezaji waliokuja England na kushindwa kufanya vizuri mapema.Kuna mifano katika klabu yetu na pia katika vilabu vingine hivyo ni jambo jema kwa Pedro kuja na kuanza kuonyesha makali yake mara moja.
Nilitegemea angecheza kwa ubora ule kwani amekuwa katika kiwango bora katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya akiwa na FC Barcelona.Amekuja akiwa fiti ana hali,ilikuwa ni jambo tu la kuelewana na wenzie.Tangu amekuja tumekuwa tukijikita zaidi katika mbinu ili aweze kuulewa mchezo wetu na sisi tuweze kuelewa kile anachotaka.Alimaliza Mourinho.
0 comments:
Post a Comment