Katika kujenga kikosi cha Simba na kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr, klabu ya Simba imemsajili mchezaji Pape Abdloulaye Ndaw kutoka klabu ya ASC Niarry Tally ya nchini Senegal kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na mchezaji Boniface Maganga kutoka Marsh Athletes Academy kwa mkataba wa miaka 2.
Simbasports.co.tz iliongea na kaimu katibu mkuu wa Simba Collin Frisch ambaye alisema kuwa wameamua kuwasajili wachezaji hao baada ya benchi la ufundi la Simba kuridhishwa na kiwango walichoonesha wachezaji hao katika kipindi ambacho walikuwa wakifanyiwa majaribio.
Kikosi cha Simba kwa sasa kipo visiwani Zanzibar katika muendelezo wa matayarisho ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara 2015/2016.
0 comments:
Post a Comment