London,England.
Kutoka gazeti la Kirusi liitwalo Gazeta habari zinasema klabu ya Arsenal iko karibu kuinasa saini ya mshambuliaji mahiri wa klabu ya Dynamo Moscow na timu ya taifa ya Urusi Alexander Kokorin.
Arsenal imemgeukia Kokorin,24 baada ya nyota wa Real Madrid Karim Benzema kukataa kuhama katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya na kusisitiza kuwa Madrid ni nyumbani kwake.
Mbali ya Arsenal vilabu vingine ambavyo vimehusishwa na Kokorin aliyeifungia Dynamo Moscow mabao 77 ni Paris St-Germain, Manchester United, Tottenham na Zenit St Petersburg.
0 comments:
Post a Comment