Barcelona,Hispania.
Wakati Everton ikijinasibu kuwa iko karibu kuinasa saini ya winga wa Dynamo Kiev ya Ukraine Andriy Yarmolenko,kutoka Hispania taarifa zinadai FC Barcelona imejiingiza katika mbio hizo na tayari iko katika mazungumzo na Kiev kwa ajili ya kumsajili winga huyo ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Pedro Rodriguez aliyejiunga na Chelsea katikati ya wiki iliyopita.
Kuondoka kwa Pedro kumeifanya FC Barcelona iwategemee makinda Rafinha Alcantara, Munir El Haddadi na Sandro Ramirez kuziba nafasi ya nyota yoyote kati ya Messi-Suarez au Neymar ikiwa watapatwa na majeruhi.
Kutoka gazeti la MACCA habari mpya zinadai kuwa tayari Dynamo Kiev imeipa muda FC Barcelona mpaka ijumaa ihakikishe kuwa imefanikisha dili hilo vinginevyo Yarmolenko atajiunga na Everton ambayo iko tayari kutoa €25m.
MAKUBALIANO MENGINE:Ikiwa makubaliano yatafikiwa juu ya uhamisho huo basi FC Barcelona itamnunua Yarmolenko kwa ada ya €20m ambayo italipwa kwa awamu tatu.Kwa kuanzia FC Barcelona italipa €5m,€5m Januari 2016 kisha €10m mwishoni mwa msimu.Pia Yarmolenko atabaki Kiev mpaka Januani mwakani kwa kuwa bado FC Barcelona inatumikia kifungo cha kuzuiwa kusajili.
0 comments:
Post a Comment