Hiki ni kipindi cha usajili barani Ulaya,Asia,Marekani , Afrika na pengine kila kona ambako soka linachezwa.Furaha kubwa kwa mashabiki wa soka huwa ni kusikia klabu yao imesajili mchezaji mpya ama yule wanayemchukia akitimka zake na kujiunga na klabu jinjine lakini linapokuja swala la klabu yao waipendayo kutangaza kuwa imeeachana na mpango/imeshindwa kumsajili nyota waliyekuwa na matumaini nae habari huwa ni tofauti sana.
Ifuatayo ni orodha ndefu ya nyota ambao bosi wa Man United bwana Ed Woodward alijaribu kutaka kuwasajili lakini mwisho wa siku akaiishia kuambulia maumivu ndani ya moyo wake baada ya ama kuzidiwa kete na vilabu vingine ama kushindwa kutoa pesa ya kutosha kuwashawishi nyota hao pamoja na vilabu vyao
Leighton Baines (Summer 2013)
Gareth Bale (Summer 2013)
Cesc Fabregas (Summer 2013)
Thiago Alcantara (Summer 2013)
Mats Hummels (Summer 2014)
0 comments:
Post a Comment