Unaikumbuka ishu ya John Terry kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wayne Bligde?Unaikumbuka pia ishu ya Ryan Giggs kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa kaka yake wa damu?
Kama umesahau basi kuna skendo nyingine inayofanana na hizo imeikumba medani ya soka baada ya nyota wa Aston Villa Jordan Ayew kubainika kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa mpenzi wa mchezaji mwenzie katika timu ya taifa ya Ghana Afriyie Acquah aitwaye Amanda.
Skendo hiyo imeibuka baada ya kuvuja kwa mkanda wa video unaodaiwa kutoka kwa Amanda ukimuonyesha mrembo huyo akikiri kufanya mapenzi na Ayew kwa kipindi cha miaka minne bila ya Acquah kugundua licha ya kuwa na Ayew katika timu ya taifa tangu mwaka 2012.
Ifuatayo ni nukuu ya kile kinachosikika katika mkanda huo "Nimekuwa na uhusiano na Jordan Ayew kwa miaka minne,siyo siku nne.Nimefanya nae mapenzi mara nyingi kuliko Acquah.Tumekuwa kama mke na mume.
Acquah ana wivu sana anaponiona niko na Ayew tukitembea au tukichati amekuwa akichukua sana mpaka nimuombe msamaha ndipo mambo yaende.Kuna wakati wakati Ayew na Acquah walikuwa safarini na timu ya taifa lakini hakuna aliyekua akiongea na mwenzie zaidi ya Dede Ayew [Kaka wa Jordan].Kuna wakati Jordan aliwahi kumuomba namba ya simu Acquah lakini alinyimwa.Mwisho wa kunukuu.
Baada ya kuibuka kwa skendo hiyo habari za ndani toka katika kambi ya timu ya taifa ya Ghana taarifa zinadai kuwa nyota wa zamani wa timu hiyo Augustine Arhinful amemtaka kocha wa timu hiyo Avram Grant kuwaondoa kikosini nyota hao ili kutoivuruga timu.
0 comments:
Post a Comment