728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 30, 2015

    SINEMA YA VICTOR WANYAMA NA SOUTHAMPTON YACHUKUA SURA MPYA,YAFURAHISHA YAKERA

    Victor Wanyama anataka kuihama Southampton na kujiunga na Tottenham.Southampton haitaki Victor Wanyama aondoke.Hii ndiyo sinema inayoendelea huko St.Mary's.

    Baada ya Wanyama kuiambia Southampton kuwa anataka kuhama na kwenda Tottenham kuungana na kocha wake wa zamani Mauricio Pochettino,hali ya mambo ndani ya klabu hiyo imezidi kuchukua sura mpya baada ya kiungo Victor Wanyama kuondolewa katika kikosi kitakachovaana na Watford jumapili ya leo.

    Tukio hili ni la pili baada ya Wanyama kuukosa mchezo wa alhamisi wa michuano ya Europa Ligi ambapo Southampton ilitupwa nje ya michuano hiyo na FC Midtjylland kwa madai kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo lakini habari za hivi punde zinadai kiungo huyo alikuwa mzima wa afya lakini alitemwa kwa makusudi kikosini kama njia ya kumkata makali ya kutaka kuhama.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SINEMA YA VICTOR WANYAMA NA SOUTHAMPTON YACHUKUA SURA MPYA,YAFURAHISHA YAKERA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top