MCHEZO KWA UJUMLA
Hatimaye Chelsea imepata ushindi wake wa kwanza wa ligi kuu baada ya leo jumapili mchana kuibuka na ushindi wa bao 3-2 ugenini dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Hawthorns.
Chelsea ilipata bao lake la kwanza dakika ya 20 kupitia kwa nyota wake mpya Pedro aliyegongeana vizuri na Eden Hazard bao la pili likifungwa na Diego Costa dakika ya 30 akiunganisha pasi ya Pedro huku bao la tatu likifungwa dakika ya 42 na mlinzi Cesar Azpilicueta aliyeuwahi mpira uliokuwa ukiambaa eneo la hatari,West Brom wao wakipata mabao yao dakika za 35 na 54 kupitia kwa kiungo James Morrison ambaye kabla ya mabao hayo alikosa bao dakika ya 14 baada ya mkwaju wake wa penati kuokolewa na mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois.Penati hiyo ilipatikana baada ya kiungo Nemanja Matic kumuangusha katika eneo la hatari winga msumbufu Callum McManaman.
KADI NYEKUNDU
Chelsea ilipata pigo dakika ya 58 baada ya nahodha na mlinzi wake John Terry kulimwa kadi nyekundu baada ya kumndondosha nje kidogo ya eneo la hatari mshambuliaji wa West Brom Solomon Rondon.
VIKOSI
WEST BROM (BAGGIES) Myhill, Dawson, McAuley, Olsson, Brunt, McManaman, Morrison, Fletcher (c), Yacob, McClean, Rondon.
Subs Rose, Chester, Lescott, Gardner, Gnabry, Anichebe, Lambert.
CHELSEA (BLUE) Courtois; Ivanovic, Zouma, Terry (c), Azpilicueta; Matic, Fabregas; Pedro, Willian, Hazard; Diego
Costa. Subs Begovic, Cahill, Mikel, Loftus-Cheek, Traore, Remy, Falcao.
0 comments:
Post a Comment