Chelsea imemgeukia mlinzi Zhang Linpeng wa Guangzhou Evergrande ya China baada ya kutoswa na Everton katika harakati za kutaka kumsajili mlinzi wake John Stones.Zhang Linpeng, 26 anafananishwa kiuchezaji na mlinzi wa Real Madrd Sergio Ramos kwa mujibu wa kocha Muitaliano Marcello Lipp,i Linpeng ndiye mchezaji bora zaidi katika ligi ya China.
Linpeng alijiunga na Guangzhou mwaka 2010 na kufanikiwa kushinda mataji manne ya ligi ya China huku akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 13 na kutengeneza 21 katika michezo 144.
0 comments:
Post a Comment