728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 22, 2015

    ARSENAL YAMALIZANA NA KARIM BENZEMA

    Arsenal kumtambulisha Karim Benzema kabla ya mchezo wake ligi kuu dhidi ya Liverpool utakaopigwa siku ya jumatatu katika dimba la Emirates.

    Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa gazeti la michezo la Italia la Gazzetta dello Sport aitwaye Emanuele Giulianelli.Giulianelli ana amini Benzema atafanyiwa vipimo vya afya mapema siku ya jumatatu kabla ya kutambulishwa usiku mbele ya mashabiki wa Arsenal.

    Giulianelli ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa "Arsenal wamekodi ndege binafsi itakayo safiri kwenda kumleta Benzema siku ya jumapili jioni.

    "Atafanyiwa vipimo jumatatu mchana kabla ya kutambulishwa baadae katika mchezo dhidi ya Liverpool"Alimaliza Giulianelli.

    Taarifa hii ya Giulianelli imekuja siku moja baada ya mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya QPR na Fulham Rodney Marsh kudai kuwa Real Madrid wamekubali kumuuza Benzema kwenda Arsenal kwa ada inayodhaniwa kuwa ni £48m. 





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAMALIZANA NA KARIM BENZEMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top