Hatimaye kiungo Asier Illarramendi ameamua kurudi nyumbani Real Sociedad (La Real) baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid.
Madrid "Los Blancos" imeamua kumuuza Illarramendi kwa ada pungufu ya €17m ikiwa ni misimu miwili tu tangu imnunue toka Real Sociedad kwa kitita cha €32m mwaka 2013.
Illarramendi,25 amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea miamba hiyo ya Anoeta inayonolewa na kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes.
Akiongea baada ya kutambulishwa mbele ya mashabiki lukuki waliojitokeza katika dimba la Anoeta kumuunga mkono Illarramendi amesema "Siku zote nimekuwa nikiota kurudi La Real.Nimefurahi kurudi tena nyumbani".
Wakati Real Sociedad wakifurahia uhamisho huo upande wa pili Liverpool wao wanaugulia maumivu ya kumkosa kiungo huyo ambaye wamemfukuzia kwa kipindi kirefu sasa.
0 comments:
Post a Comment