Wakati Yaya Toure akitamka kuwa anataka kupumzika kuichezea timu yake ya taifa kwa kipindi fulani na kuwekeza akili na nguvu zake kuipigania klabu yake ya Manchester City masikio ya kocha wa Ivory Coast Michel Dussuyer hayakuwa yamefungwa.Yalikuwa wazi yakimsikiliza nyota huyo wa safu ya kiungo.
Sasa Michel Dussuyer nae amejibu mapigo baada ya kumtema katika kikosi chake nyota huyo wa zamani wa FC Barcelona ya Hispania katika kikosi cha Ivory Coast kitakachovaana na Sierra Leone Septemba 6 huko Lagos,Nigeria katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Africa ya 2017 huko Morocco.
Mbali ya Yaya Toure nyota mwingine aliyetemwa katika kikosi hicho ni mlinzi wa kushoto Siaka Tiene.
Kikosi kamili
Makipa: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe, DR Congo), Badra Ali Sangare (ASEC Mimosas), Sayouba Mande (Stabaek, Norway)
Walinzi: Jymoh Sheriff (Athletic Adjamé), Deli Simon (Slavia Prague, Czech Republic), Bakayoko Mamadou (St Truiden, Belgium), Bailly Eric Bertrand (Villarreal, Spain), Aurier Serge (Paris SG, France), Kessie Franck (AC Cesena, Italy), Adama Traore (FC Basel, Switzerland), Ousmane Viera (Rizespor, Turkey)
Viungo: Akpa Akpro Jean Daniel (Toulouse, France), Diomandé Ismael (St Etienne, France), Serge N'Guessan Yao (AFAD Djékanou), Sere Die Geoffrey (Vfb Stuttgart, Germany), Jean Michael Seri (Nice, France)
Washambuliaji: Seydou Doumbia (CSKA Moscow, Russia) , Grevinho (AS Roma, Italy), Alain Gradel Max (Bournemouth, England), Salomon Kalou (Hertha Berlin, Germany), Giovanni Sio (Rennes, France), Thomas Toure (Bordeaux, France)
0 comments:
Post a Comment