Javier Hernandez "Chicharito" ameihama Manchester United na kujiunga na Bayer Leverkusen kwa ada ya paundi 12m.Amesaini miaka mitatu.
Jakub Blaszczykowski ameihama Borussia Dortmund na kujiunga na Fiorentina kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja.
Brown Ideye,26 ameihama West Brom na kujiunga na Olympiakos ya Ugiriki
Song:Alex Song amejiunga tena na West Ham kwa mkopo akitokea FC Barcelona huku kukiwa na nafasi ya kuurefusha zaidi uhamisho huo.
Anders Lindegaard ameihama Manchester United na kujiunga na West Brom kwa mkataba wa miaka miwili.
Emanuele Giaccherini,30 ameihama Sunderland na kujiunga na Bologna ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja.
Kiungo Mbrazil Hernanez ameihama Inter Milan na kujiunga na Juventus kwa kitita cha paundi milioni 11.
0 comments:
Post a Comment