Dar es salaam,Tanzania.
Yanga FC imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo mkali na uliojaa ubabe uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Magoli ya Yanga yaliyopeleka simanzi Msimbazi yamefungwa na Hamis Tambwe kwa shuti kali la mguu wa kushoto katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza huku lile la pili likifungwa kwa kichwa na Malimi Busungu dakika ya 80 akiunganisha vyema mpira wa kurushwa wa mlinzi Mbuyu Twite ambaye baadae alilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Matokeo mengine ligi kuu bara
JKT Ruvu 0-1 Stand United (Elias Maguli)
Coastal Union 0-0 Mwadui FC
Mtibwa 0-0 Majimaji
Prisons 1-0 Mgambo FC
0 comments:
Post a Comment