728x90 AdSpace

Tuesday, September 22, 2015

MASHABIKI YANGA WAMLILIA COUTINHO

MASHABIKI wa Yanga wamemlilia kiungo mshambuliaji wao, Mbrazil Andrey Coutinho, wakiliomba benchi lao la ufundi kumpa nafasi badala ya kumng’ang’ania Geoffrey Mwashiuya ambaye anaonekana kupoteza umakini wake.

Mashabiki hao walionekana wazi kuvikosa vitu adimu vya Mbrazil huyo ambaye msimu uliopita alicheza kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza baada ya mchezo kati ya Yanga na JKT Ruvu Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mmoja wa mashabiki wa timu hiyo, Jumanne Juma, alisema Coutinho bado ni muhimu kwenye kikosi cha Yanga ukizingatia wachezaji wanaocheza naye nafasi moja hawajamzidi kiwango.

Alisema ukiwaangalia wachezaji kama Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya ambao Kocha Hans van der Pluijm amekuwa akiwatumia nafasi ya kiungo wa pembeni kushoto, bado hawajaweza kumzidi Coutinho.


(Chanzo:Bingwa)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MASHABIKI YANGA WAMLILIA COUTINHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown