728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 29, 2015

    MAPYA YAIBUKA SIMBA BAADA YA KICHAPO CHA YANGA JUMAMOSI


    MAPYA yameibuka ndani ya Simba baada ya kuelezwa kuwa kikosi cha timu hiyo kilipanguliwa mara tatu kabla ya kucheza na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Hatua hiyo ilitokana na mchecheto wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr ambaye awali alitaka kumwanzisha kiungo Peter Mwalyanzi na Awadh Juma aanzie benchi kabla ya kubadili uamuzi wake huo.
    Lakini pia, Mwingereza huyo alitaka kumwanzisha mshambuliaji wa kati, Ibrahim Ajib kabla ya kubadili uamuzi wake huo na kumpanga Mussa Hassan ‘Mgosi’.

    Habari zilizopatikana kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo zilieleza kwamba, alipoona anazidi kuchanganyikiwa juu ya kikosi cha kuanza kipute hicho, Kerr aliamua kuwashirikisha wenzake na kukubaliana kuwapanga waliocheza siku hiyo.


    (Gazeti la BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAPYA YAIBUKA SIMBA BAADA YA KICHAPO CHA YANGA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top